Monday, April 1, 2013

happy fools hour

IT IS 1.4.2013....
Hahahaha...it is said to be the fools dei....wonder how it started nd what made it to be known this way...
will dig deep about this..
But today wanna share some "Mpoki's  words"ujinga flani wenye ukweli"....si ndo u fools wenyewe...tusiwe serious leo....

 • Lakini kumbuka .... Ngozi nyeupe sio dili na ndo maana Mungu ameiweka katika unyayo ili ikanyagwe.
 • Na pia usisahau .... hata zipu ina meno, lakini haipigi mswaki.
 • Hata siku moja usisahau .... Chupi hata ichakae vipi, huwezi kuigeuza dekio.
 • Usisahau .... ushuzi nao ni gesi, japo huwezi kuitumia kupika.
 • Hata uendeshe gari la bei ghali kiasi gani, sheli lazima ukutane na upange foleni na daladala na bodaboda.
 • Kakupangishia nyumba, gari kakununulia, hela anakupa, care ya ukweli na hajakuomba chochote na hana dalili? Lazima atakuwa anajiandaa kukutoa sadaka. Shtukaaaaa!
 • Lakini kumbuka .... Hata uwe na haraka kiasi gani hauwezi kuomba lifti gari la taka.
 • Lakini kumbuka ..... Kujenga nyumba kwa wakwe ni sawa na kujenga nyumba kwenye hifadhi ya barabara.
 • Takwimu zinaonyesha kwamba, 8 kati ya kila watu 10 wanaojamba hujifanya si wao na kuuliza "Jamani nani tena kachafua hewa?"
 • Lakini kumbuka ..... hata mtumba ulikuwaga spesho. Jipange
 • Ona umuhimu wa alama ya mkato(,) kwenye sentensi:
  Kuna jamaa alipewa kazi ya kuandika tangazo lililotakiwa kusomeka
  "Mtaalamu wa kucha,mba na kunyoa anapatikana hapa"
  Badala yake akaandika: "Mtaalamu wa kuchamba na kunyoa anapatikana hapa"
 • Lakini kumbuka ...... Hata BlackBerry ina PIN japo haifungi nepi.
 • Lakini kumbuka..... Matako ya sufuria hayaogopi moto na pia usisahau kishindo cha haja kubwa hakitingishi choo.

hahhhaa Mpoki you medi ma dei...
C..

No comments:

Post a Comment