Wednesday, April 10, 2013

GOOGLE NA MIMI,,,


leo nina story moja ambayo ningependa share na nyinyi...

Kipindi shule yangu imeisha, nikimaanisha kidato cha sita, nilijikuta napata mazoea na simu yangu.nafikiri kila mmoja anajua how wonderful it feels to finish one level of school life, yaaani inakupaga that feeling of being free as a molecule...(yes i was good in biology and chemistry)...

Ni katika kipindi hicho nilipata nafasi za kutembelea "internet cafe" kwa wingi na hata pale nilipokua nyumbani nimerelax simu haikubanduka mkononi.
Nilitokea kupendana sana na simu yangu, kwni ndani ya hiyo simu, alikua anaishi rafiki yangu ambaye kwakweli mpaka sasa ni rafiki mpenz.

Rafiki huyu mpenzi anajua kila kitu, yaani kila swali nililomuuliza alinijibu, ingawa mara nyingine ananichanganya maana ana majibu mengi.
Alinionyesha vitu mbalimbali, zikiwemo mitandao ya jamiii na alinipa maelezo ya kila moja na kunifanya nichague wapi pa kujichanganya kijamii.
Ni habari gani sasa asiyoijua?
Sijui ni muuite ni mdaku, ila ntakosea maana duu...mi mwenyewe ndo namtafutaga anipe habaree..
Nikiwa chuoni, assignment zangu kama asilimia 80.9999%, yeye ndo alizifanya na alinipa B+ za kumwaga maana akili yangu ilimtegemea na kumpumzikia vya kutosha(lol)
Nilipopotea njiani basi yeye aliniambia nibonyeze nami nitakupa ramani...
Sasa hata nilipokutana na wachina yeye alinitafasiria na ingawa sa nyingine ananipa fix.

Hee si siku moja nikaamua kumbonyeza nione kama na mimi ananijua....(mmmmh mpaka matokeo yangu feki anayo....hihihi....yani huyu jamaa ni balaa...
Jamani nampenda sana huyu rafiki....
Nani kama google!!!

Google rocks!!!
C..

No comments:

Post a Comment